Chris Brown baada ya kusikia Rihanna yupo single



Liwezekanalo leo lisingoje kesho na hii imetokea kwa staa maarufu  Marekani Chris Brown baada ya kuamua kumfollow aliyekuwa mpenzi wake miaka kadhaa iliyopita Rihanna baada ya kusikia tetesi kuwa staa huyo ameachana na mpenzi wake Hassan Jemeel.
Chris Brown na Rihanna waliwahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na kuachana mwaka 2013 na baadae Chris Brown kuanzisha mahusiano mapya na mwanadadaKarruche Tran na baadae wawili hao kuachana mwaka 2015 .

Kupitia mtandao huo wa instagram staa huyo hajamfollow Rihanna peke yake bali amemfollow Christina Milian ambaye ni rafiki wa karibu wa Karrueche Tran, baada yaChris Brown kuwa’follow wawili hao tetesi zinadai  kuwa huenda akarudisha mapenzi kwa Rihanna au Karrueche.

Comments