Alichosema ZaiiD kuhusu Darassa, ‘Ku-hit isiwe sababu ya kumshusha mtu’
Msanii wa muziki Bongo, ZaiiD amefunguka kuhusu ukimya wa Darassa kimuziki baada ya kufanya vizuri.

ZaiiD ambaye anatamba na ngoma yake mpya ‘Picha’ amesema kimuziki ukimya wa Darassa si kwa sababu ya kufanya vizuri sana na ngoma ya Nuziki bali kikawaida msanii yeyote kuna wimbo ambao hufanya vizuri zaidi kushinda nyingine.

“Darassa alichotoa baada ya Muziki ni muziki mzuri pia tena sana tu, ku-hit isiwe sababu ya kumshusha mtu vyeo. Ku-hit ni matokeo, kuna watu hawajui hata kuimba hapa Bongo lakini wana-hit,” amesema.
“Ku-hit wakati mwingine kunaendana na matukio, kiki, kunaendana na vitu vingi sana. Ukiona ngoma yako imeenda bila changamoto yoyote basi jua wewe ni msanii mkubwa na mzuri,” ZaiiD ameiambia Bongo5.
Utakumbuka baada ya Darassa kufanya vizuri na wimbo wake ‘Muziki’ alikuja kutoa wimbo mwingine uitwao Hasara Roho kisha kimya kirefu. Tangu August 12, 2017 hajaposti kitu chochote katika kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Comments
Post a Comment